1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUswisi

SIPRI: Mataifa ya silaha za nyuklia yaimarisha nguvu zao

12 Juni 2023

Ripoti mpya ya kila mwaka ya taasisi ya kimataifa ya utafiti wa masuala ya amani SIPRI inasema mataifa ya silaha za nyuklia yanaimarisha nguvu zao kwenye silaha hizo

https://p.dw.com/p/4SSTA
Südkorea USA Militär Manöver
Picha: South Korea Defense Ministry/AP Photo/picture alliance

Taasisi hiyo yenye maskani yake huko Sweden inasema ufadhili wa kile kinachoitwa vichwa vya nyuklia kimataifa ilipungua kwa karibu 200 hadi makadirio ya 12,512 katikati ya mwanzo wa mwaka 2022 na mwanzoni mwa 2023. Lakini kwa upande mwingine idadi ya silaha za nyuklia zenye uwezo wa kutumika ziliwekwa katika alama ya kuongezeka kwa 86 hadi wastani wa 9,576.

Marekani na Urusi katika mpango wa kina kuboresha vichwa vya nyuklia

Ripoti hiyo inayataja mataifa ya Marekani na Urusi kuwa katika mipango ya kina na yenye gharama ya kuboresha vichwa vya nyuklia, makombora, ndege, meli za kivita na viwanda vya uzalishaji silaha.

Kwa miongo kadhaa, idadi silaha za nyuklia kimataifa imekuwa ikipungua kwa kasi. Hata hivyo kupungua huko kulitokana na ukweli kwamba vichwa vya nyuklia vilianza kuteketezwa kwa taratibu na wenye idadi kubwa Urusi na Marekani.