1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Shujaa wa filamu ya Hotel Rwanda kuachiwa huru

24 Machi 2023

Paul Rusesabagina, aliyeangaziwa kama shujaa kwenye filamu ya Hollywood kuhusu vita vya Rwanda inayoitwa Hotel Rwanda, ataachiwa huru kesho Jumamosi.

https://p.dw.com/p/4PC8O
Ruanda Paul Rusesabagina
Picha: Cyril Ndegeya/Xinhua/IMAGO

Rusesabagina ambaye anatumikia kifungo cha miaka 25 jela nchini Rwanda baada ya kushtakiwa kwa makosa ya kuhusika na ugaidi alihukumiwa Septemba mwaka 2021 baada ya kukutwa na hatia ya kuwa na mahusiano na mtandao unaoupinga utawala wa   Rais Paul Kagame.

Kwa mujibu wa chanzo cha serikali ya Kigali, Rusesabagina kwanza atasafirishwa kwenda  Doha na baadaye kupelekwa nchini Marekani. Aidha chanzo hicho kimeeleza kwamba hatua ya kuachiwa kwake imekuja baada ya shujaa huyo wa Hotel Rwanda kumuandikia barua Rais Paul Kagame kuomba ahurumiwe.

Soma pia:Majadiliano yafanyika juu ya hatma ya Paul Rusesabagina

Marekani imekuwa ikisema Rusesabagina anazuiliwa kimakosa kwa sababu ya kile ilichosema ni kukosekana haki katika undeshaji wa kesi. Rusesabagina ni raia wa Rwanda mwenye ukaazi wa kudumu wa Marekani.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW