1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Majadiliano yafanyika juu ya hatma ya Paul Rusesabagina

13 Machi 2023

Rais wa Rwanda Paul Kagame amesema leo kuwa kuna majadiliano ya kutatua hatma ya Paul Rusesabagina, anayetumikia kifungo cha miaka 25 nchini Rwanda kwa makosa ya ugaidi.

https://p.dw.com/p/4Oc9a
Ruanda | Paul Rusesabagina | Prozess in Kigali
Picha: Clement Uwiringiyimana/REUTERS

Rusesabagina aliyeoneshwa kama shujaa katika filamu ya Hollywood ya "Hotel Rwanda", alihukumiwa Septemba 2021 kufuatia tuhuma za uhusiano wake na shirika linalopinga utawala wa Kagame.

Alikana tuhuma zote hizo na kukataa kushiriki katika mashtaka ambayo yeye na wafuasi wake wanayataja kuwa ghilba ya kisiasa.

Marekani imemuorodhesha kama aliyefungwa kimakosa, kutokana kwa sehemu, na kile ilichokiita ukosefu wa uhakikisho wa haki, katika usikilizaji wa kesi yake. Rusesabagina ana kibali cha kudumu cha kuishi Marekani.

Kagame amesema nchi yake haitotishwa kuhusiana na Rusesabagina, lakini leo alionekana kuashiria kwamba ipo nafasi ya muafaka.