1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ufaransa, Ujerumani zaiongezea shinikizo Rwanda kuhusu Kongo

22 Desemba 2022

Shinikizo la kimtaifa linazidi kuongezeka dhidi ya Rwanda baada ya Ufaransa na Ujerumani kuwa mataifa ya hivi karibuni zaidi kuituhumu wazi nchi hiyo kuwaunga mkono waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4LKVn
UN-Vollversammlung in New York | Treffen Macron mit Tshisekedi und Kagame
Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Kwa miezi kadhaa sasa, mashambulizi mapya ya waasi wa M23 yameighadhabisha serikali ya Kongo na kusababisha kauli za vita mashariki mwa Kongo, kanda tete lenye utajiri wa madini muhimu kwa sehemu kubwa ya teknolojia ya dunia.

Ripoti ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa mapema mwaka huuilisema walikuwa na ushahidi usiopingikakwamba vikosi vya jeshi la Rwanda vilikuwa vinaunga waasi mkono, na Marekani pia imeitaka wazi Rwanda kuacha hilo.

Sasa wafadhili wakuu wamejiunga na ukosoaji wa Rwanda. Siku ya Jumanne wizara ya mambo ya nje ya Ufaransa ilitoa taarifa ikilaani uungwaji mkono wa Rwanda kwa waasi wa M23, na waziri wake mdogo anaehusika na maendeleo wakati wa ziara nchini Kongo, alionya kwamba M23 wanapasw akuacha mapigano na kujiondoa. Waziri huyo mdogo, Chrysoula Zacharopoula, anahusika na utekezaji wa sera za misaada.

Msaada rasmi wa maendeleo  wa Ufaransa kwa Rwanda uliongezeka kutoka chini ya dola milioni 4 mwaka 2019 hadi zaidi ya dola milioni 68 mwaka 2021, kwa mujibu wa data za Shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, wakati uhusiano baina ya mataifa hayo ukiboreka.

Soma zaidi:Rwanda yasema Jumuiya ya Kimataifa inakuza mzozo wa DRC

Pia siku ya Jumanne, mkurugenzi wa kanda ya Afrika kusini mwa Jangwa katika wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, Christoph Retzlaff, aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa Rwanda inapaswa kusitisha mara moja msaada wake kwa M23 na kuchangia haraka kutatua mzozo huo mbaya. Msaada rasmi wa Ujerumani kwenye maendeleo ya Rwanda ulikuwa zaidi ya dola milioni 94 katika mwaka 2021.

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano jioni serikali ya Rwanda ilisema kuishtumu kuunga mkono waasi wa M23ni makosa, na kwamba kujaribu kushughulikia hali ngumu kwa kurudia na kukuza madai ya uongo ya serikali ya Kongo hakuwezi kuleta ufumbuzi.

'Siyo tatizo la Rwanda ni la Kongo'

Iliishtumu jamuiya ya kimataifa kwa kutokuwa tayari kuvikabili visababishi vya mzozo wa mashariki mwa Kongo, ambako makundi kadhaa ya silaha yanaendesha shughuli zake.

Vita vya M23 vinaathiri pia wakazi wa Bukavu

Rais wa muda mrefu wa Rwanda Paul Kagame, wiki iliyopita akizungumza kandoni mwa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika, alikanusha madai kwamba Rwanda imesababisha matatizo mashariki mwa Kongo na kuutaja mzozo huo kuwa tatizo la Kongo.

Lakini wasiwasi unaongezeka kwamba washirika wa kimataifa wanaweza kufuatisha maonyo yao kwa kuikatia msaada Rwanda, ambayo kwa muda mrefu imenufaika na msaada huo katika sekta za afya, ulinzi na maeneo mengine.

Ubelgiji, ambayo ni mkoloni wa zamani wa Rwanda, pia illiiomba nchi hiyo kuacha kuwaunga mkono waasi wa M23 mapema mwezi huu. Shinikizo la umma juu ya Rwanda kuhusiana na madai ya kuunga mkono kundi la M23 linaonekana dhahiri.

Mashirika ya haki za binadamu na wenginewameituhumu Rwanda kwa muda mrefu kutumia hatiaya jumuiya ya kimataifa kuhusiana na kuchelewa kwake kushughulikia mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 nchini humo, kupunguza ukosoaji wa wa matendo yake, ikiwemo kukandamiza upinzani nyumbani na nje.

Soma zaidi:Blinken airai Rwanda kuwakabili waasi Kongo

Mauaji hayo ya kimari yaliangamiza zaidi ya watu 800,000 wa jamii wa Watutsi and Wahutu wenye msimamo wa wastani waliojaribu kuwalinda, na suala hilo linasalia kuwa nyeti.

Rais wa Rwanda na serikali yake katika wiki za karibuni wameelezea wasiwasi kwa ajili ya watu wa jamii ya Watutsi mashariki mwa Kongo, ambao wameathirika na vurugu za sasa.

Kundi la M23 linaundwa kwa sehemu kubwa na wapiganaji wa jamii ya Watutsi. Limekanusha kuungwa mkono na vikosi vya jeshi la Rwanda.

Uhusiano wa panda shuka

Rwanda nayo imeishtumu Kongo kwa kuunga mkono kundi lenye silaha mashariki mwa Kongo la FDLR, ambalo ni la Wahutu wanaopinga ushawishi wa Watusti. Kongo imekanusha shutma hizo.

Felix Tshisekedi und Paul Kagame | Präsidenten DR Kongo und Ruanda
Rais wa Rwanda Paul Kagame na mwenzake wa Kongo Felix Tshisekedi Picha: SIMON WOHLFAHRT/AFP/Getty Images

Juhudi za kuleta amani zimekuwa na mafanikio kidogo wakati pande zote zinashtumiana kuvunja usitishaji mapigano ulioafikiwa mwezi Novemba nchini Angola.

Uhusiano kati ya Rwanda na Kongo umekuwa wa panda shuka kwa miongo kadhaa. Rwanda inadai kwamba Kongo ilitoa hifadhi kwa Wahutu waliofanya mauaji ya kimbari

Soma zaidi:Tshisekedi amtaja Kagame "adui" wa Kongo

Mfano moja wa umuhimu wa msaada ambao Rwanda inaendelea kuupokea kutoka kwa washirika ni euro milioni 20 kutoka Umoja wa Ulaya, uliotanagzwa mwezi huu, kusaidia operesheni za vikosi vyake dhidi ya wapiganaji wa itikadi kali kaskazini mwa Msumbiji.

Katika miaka ya 1990, Rwanda ilituma mara mbili wanajeshi wake ndani kabisaa ya Kongo, na kuungana na kiongozi wa waasi Laurent Desire Kabila kumuondoa madarakani diktetawa muda mrefu wa taifa hilo Mobutu Sese Seko. Vikosi vya Rwanda nchini Konfo vilishtumiwa pakubwa kuwasaka na kuwaua watu wa jamii ya Wahutu, wakiwemo raia.

Chanzo: AP