Licha ya kipaji cha kuandika mashairi lakini pia ni kiongozi wa kupigiwa mfano katika jamii yake inayokabiliwa na mapigano makali huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Shiko anaongoza kundi la vijana kwa kutumia sanaa kueleza hali inayoendelea katika taifa lake ya ukosefu wa usalama, lakini pia nafasi ya kijana kwenye jamii.