1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria ya watoto wahamiaji wasio halali nchini Ufaransa.

Mohammed AbdulRahman25 Mei 2006

Polisi wametakiwa kuhakikisha hadi Juni 30 watoto wanaoishi isivyo halali wanaihama nchi hiyo na Jumuiya zinazopigania haki za binaadamu zinasema sheria ya Waziri wa ndani Sarkozy ina lenga kuvutia kura za wafuasi wa mrengo wa kulia katika uchaguzi wa rais mwaka ujao.

https://p.dw.com/p/CHnI
Waziri wa ndani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy
Waziri wa ndani wa Ufaransa Nicolas SarkozyPicha: AP

Serikali za Ufaransa za vyama vyote vilivyokua madarakani, kwa miaka 15 iliopita,zimekua zikiwafukuza kwa njia moja au nyengine watoto na vijana walio wahamiaji wasio halali .

Mwaka 2004 walifukuzwa nchini kiasi ya 16,000 na idadi ikaongezeka mwaka jana hadi 20,000 na inatazamiwa kuongezeka zaidi mwaka huu kufikia 30,000.

Mariama ni binti ambaye wazazi wake wanaotaka Senegal na wanaishi kaskazini mwa mji mkuu Paris. Yeye ni miongoni mwa watoto 30,000 na vijana ambao polisi ya ufaransa imetakiwa kuwafukuza nchini au kama inavyoelezwa rasmi, “kuwasindikiza hadi mipakani.”

Kufukuzwa kwa watoto wanaoishi kinyume cha sheria, ni sehemu ya sera ilioanzishwa na waziri wa ndani Nicolas sarkozy, ambaye atagombea Urais mapema mwaka ujao. Sarkozy aliwasilisha sheria nyengine mapema mwaka huu akiweka masharti magumu kuhusu wageni wanaotaka kuishio Ufaransa.

Sheria hiyo ambayo iliidhinishwa na bunge Mei 17, inaweka ukaguzi mkali zaidi katika suala la ndoa kati ya wenye uraia wan chi mbili na usafiri kwa jamaa wa wahamiaji wanaoishi Ufaransa. Kadhalika inaweka utaratibu mpya wa kuwachagua wahamiaji.

Sarkozy anadai Ufaransa inahitaji kuawachagua wahamiaji akiwa na maana nani anastahiki kuwa mhamiaji Ufaransa badala ya kile anachokiita “kuwaingiza katika maafa”. Wakosoaji wake wanamshutumu kwamba anajaribu kuvutia kura za wafuasi wa siasa za mrengo wa kulia, kundi ambalo katika uchaguzi uliopita wa Rais lilinyakua asili mia 15 ya kura.

Katika hatua za kuipinga sheria hiyo , kuna mshikamano wa shule, makanisa na maafisa wa serikali za mitaa na sehemu kubwa ya wakaazi wa Ufaransa. Mtandao wa waalimu ujulikanao kama “Elimu bila mipaka” umeanzisha kampeni ya kuwalinda wanafunzi wa wahamiaji, ukiviwakilisha kiasi ya vyama 130 vya waalimu na wazazi . Mtandao huo umetoa tangazo lisemalo “Tutawapatia makaazi na kuwalipa” na kuwataka raia wa Ufaransa kuipinga sheria hiyo.

Wito hnuo unaelekea kuungwa mkono na wengi, licha ya kwamba sheria ya Oktoba mwaka jana inataja juu ya uwezekanao wa kuhukumiwa kifungo cha miaka 5 na faini ya hadi euro 30,000 kwa yeyote atakayemsidia mtoto mhamiaji anayeishi kinyume cha sheria Ufaransa.

Wanaharakati wanataja mifano ya hayati Rose Parks nchini Marekani. Mwanamke ambaye alisimama kidete tarehe 1 Desemba 1955, na kukataa kuheshimu sheria ambayo ingemlazimisha ainuke kitini mwake ndani ya basi, kumpa nafasi abiria wa kizungu. Kwa kufanya hivyo akageuka kichocheo cha vuguvugu la kupigania haki za raia. Rose Parks alifariki dunia Oktoba mwaka jana.

Nchini Ufaransa miongoni mawa watu maarufu wanaoipinga sheria hiyo dhidi ya watoto wahamiaji ambayo inawaatthiri watoto wa rangi zote kuanzia Afrika hadi Armenia-Ulaya mashariki,ni pamoja na mtengenezaji sinema Bertrand Tavernier, mwanamuziki Mano Solo, mchekeshaji Jacques Tardy na mtaalamu wa masuala ya elimu Philippe Merieu.

Sheria ya Sarkozy inaweka muda wa hadi Juni 30, kwa watoto wote wahamiaji kuihama Ufaransa.

Rais wa kamati ya madaktari ya kuwalinda wanaotafuta ukimbizi nchini humo Didier Fassin , ameitaja sheria hii mpya kuwa ya uovu kabisa, kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia, na amabayo itakua na athari kubwa kwa jamii na binaadamu kwa jumla.