1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Shambulizi la Ukraine laharibu daraja la Crimea: Urusi

22 Juni 2023

Shambulizi lililofanywa na Ukraine limeharibu daraja linalounganisha rasi ya Crimea na eneo la kusini mwa Ukraine ambalo kwa kiasi linadhibitiwa na Urusi

https://p.dw.com/p/4Sv6u
Ukrainekrieg Krim | Angriff auf Tschongar-Brücke | TASS-Bild
Picha: Alexander Polegenko/Tass/picture alliance

Shambulizi lililofanywa na Ukraine limeharibu daraja linalounganisha rasi ya Crimea na eneo la kusini mwa Ukraine ambalo kwa kiasi linadhibitiwa na Urusi.

Soma pia: Zelensky asema operesheni ya ´kujibu mapigo´ inajikokota

Gavana wa serikali iliyowekwa na Urusi katika rasi hiyo ya Crimea, Sergei Aksyonov, amesema kupitia ukurasa wa Twitter kwamba shambulizi hilo la jana usiku liliharibu daraja hilo la Chongar.

Daraja hilo linaiunganisha Crimea, iliyoanyakuliwa na Urusi kutoka Ukraine mnamo mwaka 2014, na mkoa wa Kherson.

Shambulizi hilo linafanywa wakati Ukraine ikifanya mashambulizi ya kushtukiza yenye lengo la kurejesha eneo linalokaliwa na majeshi ya Urusi na Crimea imekuwa ikilengwa mara kwa mara, na hasa kwa mashambulizi ya droni katika miezi ya hivi karibuni.