1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Shambulizi droni lauwa watu 5 eneo la mpakani la Urusi

29 Juni 2024

Watu watano wameuwawa katika nyumba moja nchini Urusi baada ya kushambuliwa kile kilichoelezwa ndege isiyo na rubani ya Ukraine katika kijiji cha mpakani. Miongoni mwa waliouwawa wamo watoto wawili.

https://p.dw.com/p/4hf0u
Urusi Tatarstan | Mashambulizi ya ndege isiyo na rubani ya Yelabuga kutoka Ukraine
Muonekano wa jengo lililoharibiwa kufuatia shambulio la ndege zisizo na rubani za Ukraine, huku kukiwa na shambulio la Urusi dhidi ya Ukraine, huko Yelabuga, Tatarstan, Urusi katika picha hii ya Aprili 2, 2024.Picha: Ostorozhno Novosti/REUTERS

Shambulizi hilo limetokea katika kijiji cha Gorodishche, kijiji kidogo katika eneo la Kursk la Urusi, kikiwa umbali wa mita chache kutoka katika mpaka wa taifa hilo na Ukraine. Kupitia ukurasa wake wa Telegram Gavana wa Kursk Alexei Smirnov amesema watu wengine wawili wa familia hiyo wapo katika hali mbaya baada ya kujeruhiwa vibaya.

Ukraine imeongeza mashambulizi yake katika eneo la Urusi mwaka huu, ikilenga maeneo ya nishati ambayo inasema yanachochea jeshi la Urusi, pamoja na miji na vijiji vinavyopo maeneo ya mpakani.