1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky atembelea wanajeshi katika uwanja wa Donetsk

26 Juni 2024

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amewatembelea wanajeshi wa nchi hiyo katika uwanja wa mapambano katika eneo la Donetsk ambapo amefanya mazungumzo na makamanda wa ngazi ya juu wa jeshi hilo.

https://p.dw.com/p/4hXCD
Ukraine
Zelensky atembelea wanajeshi katika uwanja wa mapambano DonetskPicha: Ukrainian Presidency/AFP

Katika mazungumzo hayo Zelensky alijadili kuhusu vita vinavyoendelea na hali ya kibinadamu nchini mwake.

Ziara hiyo imekuja siku chache baada ya Zelensky kumteua kamanda mpya wa vikosi vya pamoja Jenerali Andriy Gnatov kufuatia ukosoaji wa umma baada ya wanajeshi wa Ukraine kuonekana kuzidiwa nguvu na vikosi vya Urusi katika miezi ya hivi karibuni.

Zelensky atembelea Donetsk eneo la mstari wa mbele la vita

Ameongeza kuwa Jenerali Gnatov ana ujuzi na uzoefu unaohitajika katika uwanja wa mapambano.

Zelensky alimteua Gnatov baada ya kamanda maarufu wa kijeshi kumshtumu mtangulizi wake Yuriy Sodol kwa uzembe.