1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ujerumani yakubali kuongeza mishahara

23 Aprili 2023

Maafisa wa serikali ya Ujerumani na vyama vya wafanyakazi wamefikia makubaliano ya kuwaongezea malipo zaidi ya wafanyakazi milioni 2.5 wa sekta ya umma.

https://p.dw.com/p/4QSIH
Deutschland Potsdam | Tarifparteien einigen sich auf Kompromiss im öffentlichen Dienst
Picha: Sven Käuler/dpa/picture alliance

Chama cha wafanyakazi nchini Ujerumani kimekuwa kikishinikiza ongezeko la malipo kama ilivyo kwa mataifa mengine yanayokabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei.

Waziri wa Mambo ya Ndani Nancy Faeser amesema mapema leo wakati akitangaza mpango huo ukitangazwa kwamba, wanawajibika kuwashughulikia wafanyakazi kulingana na uwezo wao, licha ya ugumu wa bajeti.

Soma Zaidi: Migomo mipya yavuruga huduma katika viwanja kadhaa vya ndege Ujerumani

Makubaliano hayo yanahusisha malipo ya mara moja ya jumla ya yuro 3,000 kwa kila mfanyakazi na yuro 1,240 za kwanza zitatolewa mwezi Juni na yuro 220 kila mwezi hadi mwezi Februari.

Mishahara itaongezwa kwa yuro 200 ifikapo mwezi Machi, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.5.