1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Migomo yavuruga huduma katika viwanja vya ndege Ujerumani

20 Aprili 2023

Wafanyakazi katika viwanja kadhaa vya ndege Ujerumani wanafanya mgomo leo kama sehemu ya migogoro ya mishahara inayoendelea kati ya sekta ya umma na waajiri.

https://p.dw.com/p/4QLfw
Deutschland, Köln | Streik bei Eurowings
Picha: Benjamin Westhoff/REUTERS

Migomo katika viwanja vya Dusseldorf, Hamburg na Cologne/Bonn imepangwa leo na kesho, wakati wafanyakazi katika uwanja wa Stuttgart wakitarajiwa kugoma kesho.

Mgomo huo umeathiri usalama wa safari za ndege, abiria na ukaguzi wa bidhaa, pamoja na nafasi nyingine za utoaji huduma. Chama cha viwanja vya ndege ADV kimekadiria kuwa karibu safari 700 zimefutwa hatua itakayowaathiri karibu watu 100,000.

Chama cha wafanyakazi Ujerumani - Verdi na Chama cha Makampuni ya Usalama wa Anga Ujerumani wanafanya mazungumzo kuhusu marupurupu ya zamu za usiku, mwisho wa mwiki na wakati wa siku kuu. Migomo pia imepangwa kufanywa na wafanyakazi wa Kampuni ya treni ya Deutsche Bahn siku ya Ijumaa.