1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya DRC yazuia vifaa vya mawasiliano vya Ulaya

5 Desemba 2023

Vyanzo kadhaa vya habari vimeiambia AFP, kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikataa kuruhusu vifaa vya vya mawasiliano ya Satalaiti vya tume ya Umoja wa Ulaya kuingizwa kwa hofu ya kubadili matokeo ya uchaguzi.

https://p.dw.com/p/4ZoQL
DRK | Partisanen der UDPS versammeln sich  vor der Festung Lubumbashi
Picha: Paul Lorgerie/DW

Vyanzo kadhaa vya habari  vimeliambia shirika la habari la AFP, kwamba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ilikataa kuruhusu vifaa vya vya mawasiliano ya Satalaiti vya tume ya Umoja wa Ulaya kuingizwa nchini humo kutokana na khofu kwamba vifaa hivyo vingetumika kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa rais baadae mwezi huu. Vifaa vilivyozuiwa na serikali ya Kongo ni pamoja na simu na vifaa vya urahisishaji mawasiliano ya mtandao pamoja navifaa vya ufuatiliaji safari za magari, ili kuwarahisishia waangalizi kuwasiliana na timu yao ya uongozi mjini Kinshasa. Umoja wa Ulaya ulichukuwa hatua ya ghafla Novemba 26 ya kufuta ujumbe wake wa uangalizi wa uchaguzi wa Kongo ikisema imetokana na sababu za kiufundi. Hata hivyo maafisa chungunzima wameliambia shirika la habari la AFP kwamba hatua ya Umoja wa Ulaya imechukuliwa baada ya ombi lake la muda mrefu la  kutaka kibali kwaajili ya kuingiza vifaa vyake kukataliwa.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW