1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Serikali ya Brazil yadhibiti umiliki wa bunduki

22 Julai 2023

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva ametia saini amri ya kuzuia upatikanaji wa silaha kwa raia.

https://p.dw.com/p/4UG85
Brasilien Waffenbefürworter in BrasÌlia
Picha: Sergio Lima/AFP

Hatua hii ni kutaka kutengua sheria zilizochochea ongezeko la umiliki wa bunduki zilizoungwa mkono na mtangulizi wake Jair Bolsonaro.

Da Silva amechukua hatua hiyo ikiwa ni msururu wa hatua za kukabiliana na ghasia mjini Brasilia, baada ya kuripotiwa kwa visa kadhaa vya ufyetuaji risasi mashuleni. Amri ya rais huyo wa Brazil itawafanya watu  kumiliki silaha mbili pekee kwa matumizi ya ulinzi binafsi.

Soma pia: Bolsonaro ahojiwa kwa njama za kumzuwia Lula madarakani

Chini ya amri hiyo, mtu yeyote anayetaka kupata bunduki atalazimika kuthibitisha kuwa anaihitaji. Wawindaji na wanaotumia bunduki katika michezo watapunguziwa idadi ya silaha hadi sita, kutoka 30 walizokuwa wakiruhusiwa kumiliki hapo awali.

Wakati wa utawala wa Bolsonaroumiliki wa bunduki kwa matumizi binafsi uliongozeka maradufu baada ya kulegeza masharti ya umiliki wa silaha.