1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Bolsonaro ahojiwa kwa njama za kumzuwia Lula madarakani

13 Julai 2023

Rais wa zamani wa Brazil, Jair Bolsonaro, amehojiwa na polisi kuhusu tuhuma za kupanga njama za kumzuia mrithi wake, Lula da Silva, kuiongoza nchi hiyo baada ya kushindwa uchaguzi wa rais.

https://p.dw.com/p/4TocQ
Brasilien Brasilia | Prozess gegen Jair Bolsonaro
Picha: EVARISTO SA/AFP/Getty Images

Seneta Marcos do Val alieleza kuwa wakati Bolsonaro akiwa bado rais, alijaribu kuandaa mkakati huo mwezi Desemba baada ya Lula kushinda duru ya pili ya uchaguzi.

Mwenyewe, rais huyo wa zamani wa Brazil anakanusha vikali tuhuma hizo akisema hakukuwa na mpango wowote wa aina hiyo. 

Soma zaidi: 

Bolsonaro amBolsonaro arejea nyumbani Brazil kuongoza upinzani wa siasa za mrengo wa kuliaeshahojiwa mara ya nne ndani ya kipindi cha miezi mitatu kutokana na masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kesi ya vito kutoka Saudi Arabia, ghasia za baada ya uchaguzi, madai ya kughushi vyeti vya chanjo za UVIKO-19.