1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHaiti

Seneta wa zamani wa Haiti akiri kupanga njama dhidi ya Moise

11 Oktoba 2023

Seneta wa zamani wa Haiti Joseph Joel John wa umri wa miaka 52, jana alifikishwa mbele ya mahakama moja ya Marekani na kukiri kosa la kupanga njama na wenzake kumuua rais wa nchi hiyo Jovenel Moise mnamo mwaka 2021

https://p.dw.com/p/4XNUu
Mwombolezaji ashika picha ya marehemu Rais wa Haiti Jovenel Moise wakati wa hafla ya ukumbusho wake katika Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Pantheon huko Port-au-Prince, Haiti, Julai 20, 2021
Rais wa Haiti aliyeuawa Jovenel MoisePicha: Matias Delacroix/AP/picture alliance

Nyaraka hizo zilizotiwa saini na John pamoja na waendesha mashtaka, zimeonesha kuwa John alikiri kutoa magari na raslimali nyingine kufanikisha njama hiyo pamoja na kukutana na watu wengine waliokuwa na nia kama hiyo nchini Haiti na katika jimbo la Florida nchini Marekani.

Soma pia:Marekani yawakamata washukiwa wa mauaji ya Jovenel Moise

John ni mtu wa tatu kushtakiwa kwa mauaji ya Moise ya Julai 2021 katika makazi yake karibu na mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince.

Marekani ina sauti katika kesi hiyo kwa sababu njama hiyo ilipangwa kwa kiasi fulani jimboni Florida, makazi ya raia wengi wa Haiti.