1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSenegal

Upinzani nchini Senegal wazindua kampeni za urais

10 Machi 2024

Upinzani nchini Senegal unaoungwa mkono na mwanasiasa machachari Ousmane Sonko umezindua kampeni za urais jana Jumamosi huku ukiahidi kuanzisha sarafu mpya ya kitaifa.

https://p.dw.com/p/4dMTA
Bango likimuonyesha mgombea wa urais nchini Senegal Bassirou Diomaye Faye
Wafuasi wa mgombea wa muungano wa upinzani Bassirou Diomaye Faye wakiwa mbele ya nyumba ya mwanasiasa wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko, huko Keur Gorgui, Dakar mnamo Machi 10, 2024.Picha: SEYLLOU/AFP

Muungano huo wa upinzani aidha umesema utafanya makubaliano mapya ya mikataba ya madini na nishati.

Ingawa hakuna kura ya maoni ya umma nchini humo, lakini mgombea wa muungano wa upinzani Bassirou Diomaye Faye anaonekana kuleta upinzani mkali miongoni mwa wagombea 19 kwenye kinyang'anyiro hicho.

Ikiwa atachaguliwa katika uchaguzi wa urais wa Machi 24, mipango ya upinzani huenda ikaleta matokeo muhimu kwenye Umoja wa Kiuchumi na Kifedha wa mataifa manane ya Afrika Magharibi lakini pia ndani ya Senegal inayopanga kuwa mzalishaji wa mafuta baadae mwaka huu.