1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapizani wapinga kucheleweshwa uchaguzi wa rais Senegal

8 Februari 2024

Baadhi ya viongozi wa upinzani nchini Senegal wameungana kupinga hatua ya kucheleweshwa kwa uchaguzi wa urais.

https://p.dw.com/p/4c9uw
Senegal Dakar | upinzani
Maandamano ya wapinzani yakikabiliwa na mabomu ya machozi ya vyombo vya usalama mjini Dakar.Picha: Stefan Kleinowitz/AP/picture alliance

Mmoja ya wagombea hao Anta Babacar amesema hayo alipozungumza na shirika la habari la Reuters siku ya Jumatano (Februari 8) na kuainisha mpango wake wa kuipinga hatua hiyo kwenye Mahakama ya Juu zaidi ya Senegal.

Babacar anayeongoza chama cha Next Generation of Citizens, ARC, amesema kwa sasa hawataki mazungumzo, makubaliano wala kuahirishwa kwa uchaguzi na kusisitiza kwamba watasalia kwenye tarehe iliyokwishapangwa.

Macky Sall, Rais anayemaliza mihula yake miwili ya kikatiba amesema anasogeza mbele uchaguzi kutokana na mvutano juu ya orodha ya wagombea na madai ya ufisadi ndani ya mahakama.