1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Schroeder asema huenda serikali ijayo ikawa ya mseto kati ya SPD-CDU

27 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEX7

Strasbourg:

Kansela Gerhard Schroeder wa Ujerumani ameliambia bunge la Ulaya mjini Strasbourg kwamba huenda serikali ijayo nchini Ujerumani ikawa ya muungano wa vyama vikubwa baina ya chama chake cha Social Democrats na kile cha wahafidhina-Christian Democrats. Hata hivyo katika hotuba yake Schroeder alionya huenda ikachukua muda hadi kufikia makubaliano. Alisema kutopatikana mshindi katika uchaguzi mkuu wa karibuni, ni sawa na kura ya imani na mageuzi ya serikali yake. Hadi sasa hakuna kati yao,si mgombea wa CDU Bibi Angela Merkel wala Bw Schroeder aliye tayari kumuachia mwengine kuwa Kansela chini ya serikali ya mseto ya vyama vyao. Mazungumzo ya pili kati ya vyama hivyo viwili yataendelea kesho Jumatano.