1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz kukutana na Biden Ijumaa

3 Machi 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz anatarajiwa kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden baadaye Ijumaa mjini Washington.

https://p.dw.com/p/4OCy5
G7-Gipfel - Abschluss | Joe Biden und Olaf Scholz
Picha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Siku chache kabla ya ziara ya Kansela Olaf Scholz  nchini Marekani, mshauri wa masuala ya ulinzi wa Marekani Jake Sullivan,kupitia televisheni ya taifa alisema kuwa Biden alikubali kuipatia Ukraine vifaru vya kivita kwa kuwa lilikuwa ni ombi la Scholz.

Kauli ya mshauri wa masuala ya ulinzi wa Biden, Jake Sullivan, si tu kwamba inakinzana na alichokisema awali bosi wake kuwa Ujerumani haikumlazimisha kubadili maamuzi yake bali pia ni tofauti na ile ya serikali ya shirikisho. Hii ni kwasababu, msemaji wao alikwisha kukataa kuwepo kwa uhusiano wowote kati ya vifaru vya kivita vya Ujerumani na vile vya Marekani

Je Marekani imeshinikizwa

Akizungumzia hilo, mhariri mwandamizi wa jarida linaloandika kuhusu siasa za kimataifa katika baraza la mambo ya kigeni la Ujerumani Henning Hoff katika mahojiano  yake na DW amesema, mtu anapokanusha namna hiyo ni kuwa tu anataka kuepuka kuifanya Marekani ionekane kuwa haikufanya maamuzi kwa kushinikizwa.

Kwa maoni yake Hoff anasema hilo limefanikiwa na huenda ni kwa sababu Kansela Scholz ana mahusiano ya karibu na Rais Biden. Katika kipindi cha mwaka mzima wa vita ya Ukraine, Scholz alikuwa akikosolewa kwa kuwa mwenye sera za kusita sita. Kansela huyo wa Ujerumani alikataa kupeleka magari ya vita hadi Biden alipoanza kufanya hivyo.

Mhariri mwandamizi wa jarida linaloandika kuhusu siasa za kimataifa katika baraza la mambo ya kigeni la Ujerumani Henning Hoff anasema kuwa katika ngazi ya usalama, ni wazi kuwa Ujerumani haiwezi kufanya chochote bila Marekani. Lakini watu wanaonekana kudhani kuwa hilo linakwepeka kwenye Nyanja za uchumi na biashara jambo ambalo hadhani kuwa linawezekana.

Mataifa ya Umoja wa Ulaya na utegemezi kwa Marekani

Muda mfupi kabla ya kuanza kwa vita ya Ukraine, serikali ya Ujerumani ilipitisha bajeti ya Euro bilioni 100 kwa jeshi lake. Ikumbukwe kuwa kwa muda mrefu kabla ya kuanza kwa vita vya Ukraine, Rais Biden alikuwa akiiomba Ujerumani iongeze bajeti yake katika ulinzi,

Deutschland | Bundestag Bundeskanzler Scholz Regierungserklärung Zeitenwende
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Hata hivyo, vita ya Ukraine kwa mara nyingine tena imeonesha wazi namna Ujerumani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya yalivyo tegemezi kwa Marekani kwenye suala la sera za usalama. Msaada wa kijeshi na wa kifedha wa Marekani kwa Ukraine  hadi sasa ndiyo mkubwa zaidi kuwahi kutolewa na mataifa ya Magharibi  yanayoiunga mkono nchi hiyo.