1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz awasili Marekani

3 Machi 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amewasili mjini Washington ambapo anapanga kukutana na Rais wa Marekani Joe Biden kwa mazungumzo yanayotarajiwa kuangazia uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine.

https://p.dw.com/p/4OCTz
Deutschland | Bundestag Bundeskanzler Scholz Regierungserklärung Zeitenwende
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kabla ya kuondoka Scholz amesema kuwa Ujerumani imekuwa na uhusiano mzuri na Marekani na amebaini kuwa amekuwa akizungumza mara kwa mara na rais Biden na kubaini kuwa katika wakati huu hali ya kimataifa ikikabiliwa na matatizo lukuki, mawasiliano kwa njia ya simu hayatoshi.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Kansela huyo kutembelea Ikulu ya Marekani karibu miezi 15 tangu aingie madarakani.