1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz: Hakuna hatari Ukraine kushambulia ndani ya Urusi

4 Juni 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf scholz amesema haoni hatari yoyote katika kubadilika kwa msimamo wake hivi karibuni kuhusiana na kuikubalia Ukraine kutumia silaha inazopewa na Ujerumani kushambulia ndani ya Urusi.

https://p.dw.com/p/4gbfL
Viongozi wa mataifa ya Baltiki wakutana Riga
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Gints Ivuskans/AFP

Akizungumza wakati wa mahojiano na redio moja katika Jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani, Scholz amesema, ana uhakika kwamba hatua hiyo haitopelekea kutanuka kwa mzozo huo kwasababu ni hatua ya kulinda miji mikubwa kama Kharkiv.

Kansela huyo wa Ujerumani amesema uamuzi huoumefanywa kwa makini na Ujerumani na marafiki zake.

Kuelekea mwishoni mwa wiki iliyopita, msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Hebestreit ndiye aliyelitoa tangazo hilo la Ujerumani kuikubalia Ukraine kushambulia ndani ya Urusi kwa silaha za Ujerumani.

Siku moja kabla Marekani ilikuwa imetoa idhini kwa Ukraine kutumia silaha zake kwa kiwango fulani, kuishambulia Urusi ndani ya mipaka yake.