1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz atangaza nchi yake itapeleka silaha zaidi Ukraine

16 Machi 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ametangaza kuwa nchi yake itapeleka silaha zaidi nchini Ukraine, kwa mfungamano na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.

https://p.dw.com/p/4OlF8
Deutschland | Bundestag Regierungserklärung Bundeskanzler Scholz
Picha: Wolfgang Kumm/dpa/picture alliance

Scholz ameyasema hayo bungeni leo Alhamisi alipowasilisha taarifa ya serikali kuhusu mkutano wa kilele wa Umoja wa Ulaya utakaofanyika wiki ijayo.

Amesema pamoja na washirika wake wa Ulaya, Ujerumani itahakikisha kwamba Ukraine inapokea silaha na vifaa vya kujilinda. Ujerumani tayari inatoa msaada mkubwa wa silaha kwa Ukraine, kwa ajili ya kuzuia mashambulizi ya Urusi.

Viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya watajadili masuala ya ushindani wa kibiashara, nishati, na vita vya Ukraine, mjini Brussels wiki ijayo kwenye mkutano wao wa kilele.