1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asisitiza kuhusu mazungumzo ya amani kwa Ukraine

8 Septemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz, ametoa wito wa juhudi mpya za amani nchini Ukraine, na kuongeza kuwa wamekubaliana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky juu ya haja ya mkutano mpya wa amani utakaoijumuisha Urusi.

https://p.dw.com/p/4kPLE
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky (kushoto) na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kulia) wakutana kwa mazungumzo katika uwanja wa ndege wa Frnakfurt nchini Ujerumani mnamo Septemba 6, 2024
Rais wa Ukraine Volodymr Zelensky (kushoto) na kansela wa Ujerumani Olaf Scholz (kulia)Picha: Boris Roessler/AP Photo/picture alliance

Katika mahojiano yaliyorushwa kwa njia ya televisheni, Scholz amekiambia kituo cha ZDF kwamba anaamini sasa ndio wakati wa kujadili jinsi ya kufikia amani katika hali ya sasa ya vita kwa kasi ya juu.

Soma pia.Scholz akiri matokeo yaliyokipa ushindi chama cha AfD yanatia wasiwasi

Scholz anakabiliwa na shinikizo nchini mwake baada ya vyama vyote vitatu katika muungano wake wa mrengo wa kati kushindwa kwenye uchaguzi katika majimbo mawili wiki moja iliyopita, hukuvyama vinavyotafuta mahusiano bora na Urusi yakipata kura zaidi.

Chama cha mrengo wa kulia Alternative for Germany, AfD, na kingine kipya cha upinzani, BSW, vinavyopinga msaada wa kijeshi kwa Ukraine katika vita vyake na Urusi, vyote vimepata mafanikio makubwa kwenye uchaguzi huo.