1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Scholz asema Harris anaweza kushinda uchaguzi Marekani

Josephat Charo
24 Julai 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amempongeza makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris kama mwanasiasa shupavu na mchapa kazi anayeweza kushinda uchaguzi wa Marekani Novemba 5.

https://p.dw.com/p/4igiu
Marekani| Kamala Harris | Olaf Scholz
Kamala Harris na Kansela Olaf Scholz wa UjerumaniPicha: SVEN HOPPE/AFP/Getty Images

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amempongeza makamu wa rais wa Marekani Kamala Harris kama mwanasiasa shupavu na mchapa kazi anayeweza kushinda uchaguzi wa Marekani Novemba 5.

Scholz amesema amewahi kukutana na Harris mara kadhaa na anafikiri inawezekana kabisa kwamba atashinda uchaguzi lakini Wamarekani wataamua. 

Soma: Harris afanya kampeni katika jimbo la Wisconsin

Hata hivyo Scholz amesita kumuunga mkono na kumuidhinisha Harris dhidi ya mpinzani wake mgombea wa chama cha Republican Donald Trump. Scholz alikuwa muwazi kumuidhinisha rais wa Marekani Joe Biden kabla hajajiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania urais wikendi iliyopita. Biden alimuidhinisha Harris kama mgombea wa chama cha Democratic kupambana na Trump.