1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kansela Scholz asisitiza uungaji mkono kwa Ukraine

Sylvia Mwehozi
8 Juni 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amerejelea uungaji wake mkono kwa Ukraine, siku moja kabla ya Wajerumani kupiga kura kuchagua wajumbe wa bunge la Ulaya.

https://p.dw.com/p/4gosS
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz
Kansela wa Ujerumani Olaf ScholzPicha: Reuhl/Fotostand/IMAGO

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amerejelea uungaji wake mkono kwa Ukraine, siku moja kabla ya Wajerumani kupiga kura kuchagua wajumbe wa bunge la Ulaya.

Katika ujumbe kwa njia ya vidio uliochapishwa hii leo, Kansela Scholz kutoka chama cha Social Democartic SPD, alisema kuwa Urusi haitofanikiwa katika mipango yake. Ameongeza kuwa Putin anapaswa kutambua kuwa kamwe hawezi kushinda na kampeni yake ya kidhalimu na kwamba Ukraine itakuwa na amani.

Soma: Uchaguzi wa Bunge la Ulaya kudhoofisha muungano wa Scholz?

Kuelekea uchaguzi wa bunge la Ulaya utakaofanyika kesho Jumapili nchini Ujerumani, utafiti wa kura za maoni unaonesha kuwa chama cha SPD kitapata asilimia 15 ya kura, ikiwa ni takribani sawa na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia, Chama Mbadala kwa Ujerumani AfD. Ushindi huo utakiimarisha AfD kama chama cha pili kwa umaarufu Ujerumani, nyuma ya vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU.