1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

SANAA::Wakimbizi zaidi ya 100 wahofiwa kufa maji huko Yemen

27 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCF3

Inaarifiwa kuwa kiasi cha wakimbizi 100, wamekufa maji au kupotea, baada ya maharamia kuvamia boti walizokuwa wakisafiria na kuwalazimisha watu hao kujitosa baharini katika pwani ya Yemen.

Shirika la umoja wa mataifa la wakimbizi UNHCR, limesema kuwa watu 29 wamethibitshwa kufa na wengine 71 hawajulikani walipo.

Shirika hilo limesema, kuwa maharamia hao walivamia boti za wakimbizi hao wapatao 450 pamoja na mali zao na kuwalazimisha kujitosa bahari .

Kiasi cha wakimbizi 290 kutoka Somalia na Ethiopea walinusurika katika mkasa huo, ambapo wamesema kuwa wanawake na watoto walibakwa kabla ya kutoswa baharini.

Eneo walikotupwa watu hao lina papa wengi ambapo wengi wa wakimbizi hao waliliwa na papa.

Shirika hilo la wakimbizi la Umoja wa Mataifa limesema kuwa kiasi cha wakimbizi elfu 4 na mia 4 mwaka huu waliwasili katika pwani ya Yemen.