1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan Kusini

Ulaya yakanusha madai ya kuvuruga uchaguzi wa Sudan Kusini

31 Mei 2024

Ujumbe wa Umoja wa Ulaya uliopo nchini Sudan Kusini umekanusha ripoti kwamba unashughulikia hatua za kuchelewesha uchaguzi nchini humo kama inavyodaiwa na Rais Salva Kiir.

https://p.dw.com/p/4gUDC
Salva Kiir | Rais wa Sudan Kusini
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amedai kwamba mataifa yenye nguvu yananuia kuvuruga uchaguzi nchini mwakePicha: Samir Bol/ZUMAPRESS/picture alliance

Naibu Mkuu wa Ujumbe huo, Lothar Jaschke amesema wao wanaunga mkono kikamilifu mazingira yatakayowezesha uchaguzi kufanyika kwa kuzingatia katiba na haki.

Kiir amedai kwamba mataifa yenye nguvu ya Magharibi yanataka kuuchelewesha uchaguzi nchini mwake lakini hakueleza zaidi kinachofanyika.

Kiongozi huyo wa Sudan Kusini amesema atahakikisha uchaguzi unafanyika Desemba kama ilivyopangwa na ametahadharisha kwamba iwapo utaahirishwa basi hatua hiyo itazua vurugu.

Ingawa Sudan Kusini inatazamiwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza katika mwezi huo wa Desemba lakini michakato muhimu ambayo ni pamoja na katiba ya kudumu na jeshi la polisi moja kwa nchi hiyo bado havipo.