1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Safari za ndege zasitishwa Frankfurt kutokana na maandamano

25 Julai 2024

Maandamano ya wanaharakati wa mazingira nchini Ujerumani, yamesababisha kufutwa kwa safari 100 za ndege katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Frankfurt.

https://p.dw.com/p/4iimZ
Deutschland | Verdi-Warnstreiks im Luftverkehr – Frankfurt am Main
Picha: Lando Hass/dpa/picture alliance

Mamlaka zimesema, waandamanaji hao waliingia ndani ya uwanja huo na kukataa kuondoka na wengine wakavamia eneo ambako ndege huondokea.

Uongozi wa uwanja wa Frankfurt hata hivyo muda mfupi baadaye ulitangaza kuendelea tena na shughuli zake baada hali kutulia.

Hii ni mara ya pili kwa wanaharakati hao kuandamana na kutatiza shughuli wakiitaka serikali ya Ujerumani iingie makubaliano ya kimataifa ya kuachana na matumizi ya mafuta, gesi na makaa kufikia mwaka 2030.