1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda yadai mauaji ya Kishishe ni ya kutungwa na DRC

22 Desemba 2022

Rwanda jana imeituhumu serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kwa kile ilichosema ''ilitunga'' kuhusu mauaji ya watu wengi.

https://p.dw.com/p/4LJR5
DR Congo Kongolesische Jugendliche schließen sich der Armee an, um Rebellen zu bekämpfen
Picha: Benjamin Kasembe/DW

Uchunguzi wa Umoja wa Mataifa ulisema watu 131 waliuwawa na waasi wa kundi la M23.

Jana Jumatano serikali ya Rwanda ilisema mauaji ya watu wengi katika eneo la Kishishe ni taarifa ya kutungwa na serikali ya Kongo na ilisambaa kwa kasi, bila ya chombo chochote cha kuaminika kufanya uchunguzi wowote wa kutafuta ukweli na kundi la M23 likatajwa kuhusika na mauaji hayo.

Rwanda imesema kilichotokea ni mapambano ya kijeshi kati ya kundi la M23 na makundi haramu yenye silaha ambayo ni washirika wa vikosi vya jeshi la Kongo.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inaituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono M23 madai ambayo Rwanda inayakanusha.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW