1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaRwanda

Rwanda: Kumbukumbu ya miaka 29 ya mauaji ya Kimbari

7 Aprili 2023

Rwanda inaadhimisha hii leo kumbukumbu ya miaka 29 ya mauaji ya Kimbari ya mwaka 1994 ambapo Wahutu wenye msimamo mkali waliwaua watu karibu milioni moja wengi wao wakiwa ni Watutsi.

https://p.dw.com/p/4PoeT
Niederlande I Völkermord Prozess vor Gericht in Den Haag
Picha: Ben Curtis/AP/picture alliance

Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoanza April 7 mwaka 1994 na vilivyodumu kwa siku 100, vilishuhudiwa siku moja tu baada ya kudunguliwa kwa ndege aliyokuwamo rais wa wakati huyo wa Rwanda Juvénal Habyarimana pamoja na yule wa Burundi Cyprien Ntaryamira.

Soma pia: Wiki ya kumbukumbu ya mauwaji ya kimbari nchini Rwanda

Viongozi hao walikuwa wametoka kwenye mkutano wa kilele nchini Tanzania ambako walikuwa wanajadili mzozo huo wa Rwanda. Mauji ya kimbari ya mwaka 1994 ni miongoni mwa matukio mabaya zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini Rwanda.