1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rwanda imetuma wanajeshi 300 Bangui

4 Agosti 2021

Rwanda kwa mara ya kwanza imetuma wnaajeshi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati kuunga mkono juhudi za ulinzi za Umoja wa Mataifa kupitia kikosi ya MINUSCA.

https://p.dw.com/p/3yWww
Zentralafrikanische Republik | MINUSCA | Friedensmission
Picha: Florent Vergnes/AFP/Getty Images

Rwanda imewapeleka wanajeshi 300 kujiunga na walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati - MINUSCA, ambako watasaidia kuweka ulinzi kwenye barabara moja kuu inayotumika kupeleka bidhaa katika mji mkuu Bangui.

Hatua hiyo ni sehemu ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa la Machi mwaka huu kulipiga jeki jeshi la MINUSCA na kufikisha karibu askari 3,000.

Msemaji wa MINUSCA Abdoulaziz Fall amesema askari hao ndio sehemu ya kwanza ya kikosi cha Rwanda ambacho kiliwasili jana kuweka ulinzi kwenye barabara kati ya Bangui na Beloko, mji ulioko mpakani na Cameroon.

Amesema wanajeshi hao watakuwa nchini humo kwa mwaka mmoja. Askari waliobaki 450 wa Kinyarwanda watawasili mwishoni mwa mwaka huu. Mapigano katika Jamhuri ya Afrika ya Kati yamepungua tangu mwaka wa 2018, lakini nchi hiyo bado inakabiliwa na mashambulizi ya hapa na pale.