1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto auondoa mswada wa fedha kufuatia shinikizo la umma

26 Juni 2024

Rais wa Kenya William Ruto amesema hatoutia saini mswada tata wa fedha na kuuondoa kabisa, siku moja tu baada ya kushuhudiwa maandamano yaliyosababisha vifo vya na kuahidi kuzungumza na vijana kutafuta mwafaka.

https://p.dw.com/p/4hYGC
William Ruto | Rais wa Kenya
Ruto auondoa mswada wa fedha kufuatia shinikizo la ummaPicha: Luis Tato/AFP/Getty Images

Rais wa Kenya William Ruto amesema leo kuwa hatoutia saini mswada tata wa fedha na kuuondoa kabisa, siku moja tu baada ya kushuhudiwa maandamano yaliyosababisha vifo vya takriban watu 23, akiahidi kuzungumza na vijana kutafuta mwafaka. 

Rais William Ruto amechukuwa uamuzi huo kufuatia shinikizo la waandamanaji vijana waliovamia bunge jana na ambao wametishia kuchukuwa hatua nyingine zaidi wiki hii.

Gachagua: Idara ya Ujasusi yaifelisha serikali ya Kenya

Vijana nchini Kenya wanadai kuwa nyongeza mpya za ushuru zilizoainishwa kwenye mswaada wa fedha wa mwaka 2024 zitawaongezea mzigo.

Rais Ruto ametangaza hatua za kubana matumizi ili kuweza kumudu mahitaji ya serikali na taifa kwa jumla. Ruto aliyebadili kauli na kuwa mpole, alitoa pia rambirambi kwa jamaa za waandamanaji waliopoteza maisha kwenye purukushani za hapo jana.

Kiongozi wa taifa alisisitiza kuwa bado azma ya kufanya majadiliano na vijana iko palepale kwani anajali maslahi yao.