1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ruto asema maandamano ya Kenya lazima yakome

21 Julai 2024

Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amesisitiza kuwa "haki" ni hitaji la lazima kabla ya mazungumzo yoyote na serikali baada ya mapigano makali.

https://p.dw.com/p/4iYZE
Maandamano Kenya-Nairobi
Afisa wa polisi amefunikwa na wingu la vitoa machozi wakati wa maandamano ya kupinga nyongeza ya ushuru jijini Nairobi, Kenya.Picha: Daniel Irungu/EPA

Rais William Ruto akionya kwamba machafuko yanaweza "kuharibu" nchi.

Raila amependekeza kwamba kila mwathirika wa ukatili wa polisi alipwe fidia na haki itendeke kabla ya mazungumzo.

Soma pia: Rais wa Kenya amerejea sehemu kubwa ya mawaziri wa zamani

Licha ya Ruto kuondoa sera ya nyongeza ya kodi, maandamano yameendela kwa wiki kadhaa kote nchini Kenya na sasa upinzani umeitisha maandamano mapya wiki ijayo.

Leo Jumapili Ruto ameahidi kuwakomesha "waporaji" na "wauaji" ambao amesema ni "hatari na unaharibu nchi " akiongeza kwamba wanataka taifa lenye amani na utulivu, na masuala ya Kenya yatatatuliwa kwa njia za kidemokrasia.