Urusi imeonya kile ilichokiita uhasama wa ndege za Marekani
15 Machi 2023Matangazo
Washington imeilaumu Moscow kwa tukio hilo, ikikiita kitendo cha marubani wake kuwa cha kizembe, lakini Urusi imekanusha kufanya ubaya wowote.
Balozi wa Urusi mjini Washington Anatoly Antonov amesema wanatumai Marekani itajizuia kutoa uvumi zaidi katika vyombo vya habari na kukomesha kurusha ndege karibu na mipaka ya Urusi.
Soma pia:Droni ya Marekani yaanguka baharini, Urusi yaombwa maelezo
Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema droni yake ilikuwa kwenye operesheni ya kawaida wakati ilipokatizwa katika njia ya kizembe, isiyo ya mazingira mazuri na isiyokuwa ya kitaalamu.
Urusiilisema ndege hiyo ilikuwa imepoteza muelekeo ghafla.