1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wagner lasema jeshi la Urusi limeteka wilaya kadhaa Ukraine

9 Machi 2023

Mmiliki wa kundi la mamluki la Urusi, Wagner, amedai kwamba vikosi vyake vimefanikiwa katika kunyakua maeneo kadhaa katika ngome ya Ukraine ya Bakhmut ila akasema hafahamu ni lini mapigano yatakapokwisha.

https://p.dw.com/p/4OQbJ
Ukraine | Krieg | Videostill Wagner-Chef Jewgeni Prigoschin
Picha: Konkord Company Press Service/ITAR-TASS/IMAGO

Mkuu huyo wa Wagner Yevgeny Prigozhin amesema wamechukua udhibiti kamili wa wilaya zote zilizoko mashariki mwa mto Bakhmutka. Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg anasema, huenda Bakhmut ikatekwa na Urusi katika siku chache zijazo.

Majeshi ya Urusi ni sharti yapitie Bakhmut ndipo yaweze kushambulia maeneo zaidi ndani ya Ukraine na eneo la Donetsk ambalo hawana udhibiti. Maafisa wa nchi za Magharibi lakini wanasema kutekwa kwa Bakhmut hakutobadili mkondo wa vita hivyo.

Mapambano ya kuchukua udhibiti wa Bakhmut yamedumu kwa miezi sita sasa.