1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Robo tatu ya Wajerumani hawaridhishwi na serikali

11 Julai 2023

Karibu robo tatu ya Wajerumani hawaridhishwi na utendaji wa serikali yao ya sasa kulingana na utafiti wa maoni uliochapishwa na kituo cha RTL siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/4Tipv
Bundestag Kanzler Scholz
Picha: Kay Nietfeld/dpa/picture alliance

Kati ya watu 1,002 waliohojiwa, asilimia 77 wamesema hawaridishwi kabisa na serikali ya sasa katika utafiti wa maoni uliofanywa na taasisi ya utafiti ya Forsa mwanzoni mwa mwezi Julai.

Mwanzo mwa mwezi Februari mwaka 2022 kuelekea kuanza kwa serikali ya muungano, idadi hiyo ilikuwa ni asilimia 64.

Serikali ya muungano ya Ujerumani inayojumuisha chama cha Kansela Olaf Scholz cha SPD, kile cha kijanii - The Greens na Waliberali wa FDP, imekuwa madarakani tangu Disemba mwaka 2021.