1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ramallah. Wapiganaji watakiwa kurejea katika makubaliano ya kusitisha mapigano.

17 Julai 2005
https://p.dw.com/p/CEtw

Rais wa Palestina Mahmoud Abbas amewataka wapiganaji kusitisha mashambilizi yao dhidi ya Israel na kurejea katika makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyodumu kwa muda wa miezi mitano.

Wito huo wa Bwana Abbas unakuja baada ya viapo vya kulipiza kisasi dhidi ya Israel vinavyotolewa na makundi ya wapiganaji wa Kipalestina.

Maafisa wa Israel wamesema kuwa wapiganaji hao wameshambulia nyumba moja katika makaazi ya walowezi wa Kiyahudi ya Nissanit katika eneo la Gaza kwa makombora yaliyotengenezwa kienyeji.

Wamesema kuwa watu wawili wamejeruhiwa kidogo.

Siku ya Ijumaa, Israel imewauwa wanachama saba wa kundi la wapiganaji wa Hamas , wakisema kuwa ilibidi kuchukua hatua hiyo kusitisha mashambulizi dhidi ya Israel.