1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Zelensky kuzuru Marekani wiki ijayo

Sylvia Mwehozi
15 Septemba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzuru Marekani wiki ijayo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Washington. Ziara hiyo itafanyika wakati bunge la Marekani likijadili msaada zaidi kwa Ukraine.

https://p.dw.com/p/4WMUD
Ukraine Kiew | Videoansprache von Wolodymyr Selenskyj
Picha: president.gov.ua

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anatarajiwa kuzuru Marekani wiki ijayo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Washington. Ziara yake inakuja wakati bunge la Marekani likijadili msaada mpya kwa Ukraine wenye thamani ya dola bilioni 21, na wiki moja baada ya waziri wa mambo ya nje Antony Blinken kutangaza kifurushi kingine cha msaada wa dola bilioni 1.

Kwingineko, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock ametoa wito wa mshikamano na Ukraine wakati wa ziara yake nchini Marekani. Baerbock alikutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya wabunge wa Republican.

Alipoulizwa jinsi mzozo huo unavyoweza kumalizika, mwanasiasa huyo wa Ujerumani alisema ni kwa uhuru na amani kwa Ukraine akiongeza kwamba wataiunga mkono Kyiv kadri inavyohitajika.