1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBrazil

Rais Xi ahimiza amani Ukraine na usitishaji mapigano Gaza

21 Novemba 2024

Kiongozi wa China Xi Jingping ametoa wito wa kuwepo miito zaidi ya kumaliza vita vya Ukraine na kusitishwa mapigano Gaza. Xi ameyasema hayo wakati akifanya ziara ya kiserikali katika mji mkuu wa Brazil, Brasilia

https://p.dw.com/p/4nEB6
Lula da Silva na Xi Jinping
Ziara ya kiserikali ya Xi inadhihirisha uhusiano wa karibu kati ya madola makubwa kiuchumi ya Asia na Amerika KusiniPicha: Ricardo Stuckert/PR

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva aliunga mkono kauli hizo wakati alikutana na Xi na akasisitiza kuhusu ramani ya pamoja ya kupatikana amani nchini Ukraine ambayo wanaipendekeza. Lula alisema katika ulimwengu uliogubikwa na migogoro ya kivita na kisiasa, China na Brazil zinaweka mbele amani, diplomasia na mazungumzo.

Ombi la rais wa China la kusitishwa vita huko Gaza -- ambako Israel inaendeleza mashambulizi dhidi ya Hamas -- liliongeza kwa kauli alizotoa pamoja na viongozi wengine wa G20 wakati wa mkutano wa kilele uliofanyika Jumatatu na Jumanne mjini Rio.

Taarifa ya pamoja na mkutano huo ilitoa wito wa mpango mpana wa usitishwaji mapigano Gaza na Lebanon, ambako Israel inaendesha operesheni dhidi ya kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran. Ziara ya kiserikali ya Xi nchini Brazil inadhihirisha uhusiano wa karibu kati ya madola hayo makubwa kiuchumi katika mabara ya Asia na Amerika Kusini.