Mkutano wa G20 wahitimishwa Brazil
20 Novemba 2024Hatua ya Marekani kuiruhusu Ukraine kutumia makombora yake ya masafa marefu kushambulia miundombinu ya kijeshi ndani ya Urusi imeibua wasiwasi kwa washirika wa Ukraine barani Ulaya, hasa baada ya Urusi kutishia kutumia silaha zake za nyuklia.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtaka mwenzake wa China Xi Jinping kutumia ushawishi wake kwa kiongozi wa Urusi Vladimir Putin. China na Brazil wamesema wanaunga mkono njia ya mazungumzo ili kuumaliza mzozo huo.
Mkutano huo wa siku mbili wa G20 , ulihitimishwa na ombi la Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva kwa viongozi wenye nguvu zaidi duniani kuchukua hatua za kuwezesha kufikiwa makubaliano kwenye mazungumzo yaliyokwama katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa wa hali ya hewa wa COP29 huko Azerbaijan.