1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Senegal ahairisha uchauzi kwa muda usiojulikana

Hawa Bihoga
4 Februari 2024

Rais Macky Sall wa Senegal ametangaza kuhairishwa kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 25 kwa muda usiojulikana, kwa kile alichokitaja kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya madai ya rushwa miongo mwa wagombea.

https://p.dw.com/p/4c1cn
Dakar, Senegal | Rais Macky Sall
Rais wa Senegal Macky Sall akitangaza kwenye televisheni kufutwa kwa uchaguzi wa FebruariPicha: RTS/Reuters

Sally hakutoa tarehe maalu ya uchaguzi lakini amesema kwamba majadiliano ya kitaifa yatafanyika ili kuhakikisha uchaguzi unakuwa huru, wa wazi na shirikishi.

Baraza la Katiba la nchini humoliliwaondoa baadhi ya wagombeakwenye orodha kutokana na sababu za kisheria, wakiwemo wanasiasa maarufu wa upinzani wanaowania nafasi ya urais Ousmane Sonko na Karim Wade, hatua ambayo imezusha mvutano wa kisiasa nchini humo.

Soma pia:Ousmane Sonko afutwa kwenye orodha ya kugombea urais nchini Senegal

Kufuatia kuhairishwa kwa uchaguzi huo wa rais, ubalozi wa Ujerumani mjini Dakar umeonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika kwa maandamano.