1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Joe Biden hatohudhuria mkutano wa COP28 Dubai

27 Novemba 2023

Rais wa Marekani Joe Biden hatohudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira utakaofanyika Dubai.

https://p.dw.com/p/4ZVCN
Kiongozi | Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe BidenPicha: Stephanie Scarbrough/AP/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden hatoshiriki mkutano wa kilele kuhusu mazingira utakaofanyika Dubai wiki hii.

Wajumbe takriban 70,000 wakiwemo viongozi wa nchi pamoja na kiongozi mkuu wa kanisa katoliki Papa Francis wanatarajiwa kushiriki mkutano huo wa COP28 utakaofunguliwa Alhamisi ambao huenda ukawa ndio mkutano wa kilele mkubwa zaidi wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira kuwahi kufanyika.

Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu sababu za Rais Biden kutohudhuria COP28.

Soma pia:Marekani na China zafikia 'maelewano' kuhusu tabia nchi kuelekea mazungumzo ya COP28

Kwa mujibu wa afisa mmoja aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa jina, serikali ya Biden bado iko kwenye majadiliano kuhusu ikiwa itatuma afisa wake wa ngazi ya juu kwenye mazungumzo hayo ya Dubai.

Mjumbe anayehusika na mazingira nchini Marekani na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nje  John Kerry ataongoza mashauriano ya  kila siku kwa niaba ya nchi hiyo.

Ujerumani yaahidi euro bilioni mbili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW