1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mkuu wa majeshi Guinea Bissau afutwa kazi

4 Desemba 2023

Rais Umaro Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau amesema tukio la makabiliano ya risasi katika mji mkuu wa Bissau siku ya Ijumaa (Disemba 1) lilikuwa ni jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4Zk8K
Rais Umaro Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau akiwatembelea wanajeshi baada ya makabiliano ya Ijumaa (Disemba1).
Rais Umaro Sissoco Embalo wa Guinea-Bissau akiwatembelea wanajeshi baada ya makabiliano ya Ijumaa (Disemba1).Picha: Privat

Kiongozi huyo amesema hayo baada ya mkutano na vikosi vya usalama, ambapo alithibitisha kutokea kwa tishio hilo ambalo ni sehemu ya matukio yanayohujumu demokrasia katika eneo la Afrika Magharibi lililokumbwa na mapinduzi ya kijeshi.

Wiki iliyopita, kikosi cha wanajeshi kiliwatoa kizuizini bila ya kufuata utaratibu wa kisheria mawaziri wawili waliokuwa wamezuiliwa na polisi kwa tuhuma za rushwa, na kusababisha makabiliano ya risasi na vikosi maalum vya ulinzi wa rais.

Soma zaidi: Hali ya utulivu yarejeshwa nchini Guinea-Bissau

Jeshi la ulinzi la taifa Guinea-Bissau limewaachilia maafisa wawili wa serikali waliokuwa wanashikiliwa kwa mahojiano kufuatia ufyatulianaji risasi
 

Wakati wa ziara katika kamandi ya wanajeshi wa ulinzi wa taifa mjini Bissau, Embalo alieleza kuwa mkuu wa majeshi Victor Tchongo ameachishwa kazi na kwamba "atalipa kwa gharama kubwa" kwa jaribio lake la mapinduzi.

Jaribio hilo la mapinduzi ni la pili katika eneo la Afrika Magharibi na Kati ndani ya muda wa wiki moja baada ya jaribio lengine lililoshindwa la wiki iliyopita nchini Sierra Leone.