1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaVisiwa vya Comoros

Rais wa Comoro ampatia mwanae wa kiume wadhifa serikalini

2 Julai 2024

Rais wa Comoro Azali Assoumani amemteua mwanae wa kiume Nour El Fath kuwa mratibu wa masuala ya serikali katika mabadiliko ya baraza la mawaziri.

https://p.dw.com/p/4hm7W
Uchaguzi wa Comoro 2024 | Rais Azali Assoumani
Rais wa Comoro Azali Assoumani alipokuwa katika harakati za kampeni kuelekea uchaguzi wa urais.Picha: REUTERS

 Assoumani alitangaza bazara lake la mawaziri Jumatatu jioni ambamo pia alimteuwa Ibrahim Mohamed Abdou Razakou kuwa Waziri wa Fedha, Said Omra Houmadi kuwa Waziri wa Sheria na kumrejesha Yousoufa Mohamed Ali katika wadhifa wa Waziri wa Ulinzi.

Wachambuzi wa kisiasa, viongozi wa upinzani na vyombo vya habari vya nchini humo wanasema  Assoumani alionekana kumuandaa El Fath mwenye umri wa miaka 40 kuchukua nafasi yake.

El Fath ni msomi aliyebobea kwenye masuala ya fedha na aliyefanya kazi kama mshauri mwandamizi wa kiuchumi wa rais huyo tangu 2019.