1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya Juu ya Komoro yathibitisha ushindi wa Azali

24 Januari 2024

Mahakama ya Juu ya Comoro imethibitisha kuchaguliwa tena Rais Azali Assoumani, ambaye ushindi wake katika uchaguzi wa wiki iliyopita ulipingwa kwa maandamano ya upinzani yaliyosababisha vifo na majeruhi.

https://p.dw.com/p/4bdhj
Azali Assoumani, Komoro
Rais Azali Assoumani wa Komoro amethibitishwa kushinda uchaguzi tena visiwani humo.Picha: Ludovic Marin/AFP/Getty Images

Rais wa kitengo cha katiba na uchaguzi katika mahakama hiyo, Rafik Mohamed, alisema siku ya Jumatano (Januari 24) kwamba Assoumani alikuwa ameshinda kwa asilimia 57.2 ya kura.  

Hata hivyo, viongozi wa upinzani wameyakataa matokeo hayo wakisema kura hiyo ilijawa na udanganyifu.