1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais wa Bolivia akanusha madai ya kula njama ya mapinduzi

28 Juni 2024

Rais wa Bolivia Luis Arce amekanusha madai ya kula njama na mkuu wake wa zamani wa jeshi aliyekamatwa baada ya mkuu huyo wa zamani wa jeshi kupeleka wanajeshi na vifaru katikati mwa mji mkuu La Paz.

https://p.dw.com/p/4heIh
Rais wa Bolivia Luis Arce
Rais wa Bolivia Luis ArcePicha: Mateo Romay Salinas/Anadolu/picture alliance

Rais wa Bolivia Luis Arce amekanusha madai ya kula njama na mkuu wake wa zamani wa jeshi aliyekamatwa baada ya mkuu huyo wa zamani wa jeshi kupeleka wanajeshi na vifaru katikati mwa mji mkuu La Paz, na kujaribu kuuvunja mlango wa Ikulu.

Akionekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu alipotangaza jaribio la mapinduzi, Arce amekanusha madai ya kula njama na Juan Jose Zuniga. Mkuu huyo wa zamani wa jeshi alidai kwamba alikuwa anafuata amri ya juu na kudai kuwa rais alitaraji jaribio hilo la mapinduzi lingemuongezea umaarufu. Viongozi wa jeshi Bolivia wakamatwa, jaribio la mapinduzi

Kiongozi huyo amewaambia waandishi wa habari kuwa, raia 14 waliojaribu kuzuia jaribio hilo la mapinduzi wamejeruhiwa kwa risasi.

Mamlaka iliwaanika washukiwa wa jaribio hilo mbele ya vyombo vya habari jana Alhamisi, na kutangaza kukamatwa kwa watu 17 akiwemo mkuu huyo wa jeshi Juan Zuniga.

Polisi wameshika doria katika majengo mbalimbali ya serikali siku moja tu baada ya jaribio hilo la mapinduzi lililofeli.