1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaBolivia

Viongozi wa jeshi Bolivia wakamatwa, jaribio la mapinduzi

27 Juni 2024

Maafisa wawili wa ngazi za juu wa jeshi wamekamatwa kufuatia tukio la wanajeshi na vifaru kuvamia eneo la majengo ya serikali katika kile ambacho Rais Luis Arce amekiita jaribio la mapinduzi.

https://p.dw.com/p/4hZaV
Mkuu wa majeshi ambaye sasa amefutwa kazi, Jenerali Juan Jose Zuniga, alisema vikosi hivyo vya jeshi vilikuwa na lengo la kuijenga upya demokrasia.
Mkuu wa majeshi ambaye sasa amefutwa kazi, Jenerali Juan Jose Zuniga, alisema vikosi hivyo vya jeshi vilikuwa na lengo la kuijenga upya demokrasia.Picha: JORGE BERNAL/AFP/Getty Images

Wanajeshi waliingia na vifaru vyao katika bustani ya kihistoria ya Murillo, ambako ndiyo yaliko makaazi ya rais na jengo la bunge, hatua iliyokosolewa kama shambulizi dhidi ya demokrasia.

Mkuu wa majeshi ambaye sasa amefutwa kazi, Jenerali Juan Jose Zuniga, alisema vikosi hivyo vya jeshi vilikuwa na lengo la kuijenga upya demokrasia.

"Tunataka kuirekebisha demokrasia. Imetosha kuongozwa na watu wachache. Tizama walipotufikisha. Watoto wetu hawajui kesho yao. Watu wetu hawajui kesho yao. Na si kwamba jeshi letu halina nguvu ya kuhakikisha kesho ya watoto wetu, mustakabali wa watoto wetu, ustawi na maendeleo ya watu wetu," amesema jenerali wa Jeshi, Juan Jose Zuniga.

Jenerali huyo pamoja na mkuu wa jeshi la maji la Bolivia, Juan Arnez Salvador, walikamatwa jana Jumatano kwa tukio hilo.

Urusi imelaani jaribio hilo na kuonya dhidi ya uingiliaji wa nje unaolivuruga taifa hilo la Amerika ya Kusini.