1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Zelenskiy atoa wito wa msaada zaidi wa silaha

26 Oktoba 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ametoa wito wa msaada zaidi wa silaha wakati taifa hilo likiendelea kujitetea dhidi ya Urusi baada ya majengo katika kinu cha nyuklia cha Khmelnytskyi kushambuliwa.

https://p.dw.com/p/4Y2KO
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameyatolea mwito mataifa ya magharibi kuisaidia silaha zaidi ili kumdhibiti Urusi
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy ameyatolea mwito mataifa ya magharibi kuisaidia silaha zaidi ili kumdhibiti UrusiPicha: president.gov.ua

Amesema shambulizi kwenye kinu hicho cha nyuklia kwa mara nyingine linawakumbusha wao na washirika wao juu ya umuhimu wa kuimarisha ulinzi wa angani.

Zelenskiy amesema hayo katika ujumbe wa video jana jioni na kuongeza kuwa shambulizi hilo linaonyesha namna Urusi inavyoweza kukwepa vikwazo kirahisi kwa kutumia baadhi ya vifaa vya magharibi kwenye droni na makombora yake.

Shambulizi hilo lilisababisha vifo vya watu 16 na wengine 20 kujeruhiwa.