1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Steinemeier ashuhudia ubunifu wa vijana wa Tanzania

31 Oktoba 2023

Rais Frank- Walter Steinmeir wa Shirikisho la Ujerumani amehudhuria maonesho ya teknolojia bunifu zinazoongozwa na vijana wa Kitanzania wakati wa ziara yake ya siku mbili iliyoanza tarehe 31 Oktoba nchini humo.

https://p.dw.com/p/4YFPv
Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani (kushoto) akiwa na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.
Rais Frank-Walter Steinmeier wa Ujerumani (kushoto) akiwa na mwenyeji wake, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Rais Steinmeir alitembelea kituo cha teknolojia ya uzalishaji wa funza kwa kutumia taka na baadaye funza hao kutumika kama chakula cha mifugo kinachoendeshwa na kampuni ya BioBuu.

Soma zaidi: Steinmeier ziarani Tanzania

Kadhalika, akiwa jijini Dar es Salaam alijionea uvumbuzi wa kijana wa Kitanzania anayesomea mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Tiba cha Muhimbili, Shabani Busega, ambaye ameunda programu ya afya inayotumia akili bunifu itakayosaidia kufanya uchunguzi wa macho kabla ya kwenda hospitali.

Soma zaidi: Steinmeier aondoka Ujerumani kuelekea Tanzania

Busega alisema anatamani Tanzania iwe sehemu ya utalii wa tiba hasa matibabu yanayohusisha teknolojia.