1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier aondoka Ujerumani kuelekea Tanzania

30 Oktoba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameondoka Ujerumani Jumatatu kuelekea Afrika kwa ziara ya siku nne.

https://p.dw.com/p/4YCEO
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kufanya ziara ya siku nne barani Afrika akianzia Tanzania Jumanne ya Oktoba 31, 2023.
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier kufanya ziara ya siku nne barani Afrika akianzia Tanzania Jumanne ya Oktoba 31, 2023.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Frank-Walter Steinmeier analenga kutanua mahusiano ya kiuchumi yaliyoko na kuanzisha mengine mapya.

Katika ziara yake hiyo ya Tanzania na Zambia, Steinmeier ataandamana na ujumbe wa kibiashara.

Siku ya Jumanne Steinmeier atakutana na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan mjini Dar es Salaam.

Suluhu aliyechukua madaraka Machi 2021, amepongezwa na serikali ya Ujerumani kwa kuulinda upinzani nchini humo na dhamira yake katika utawala wa kisheria na haki za binadamu.

Katika ziara hiyo, rais huyo wa Ujerumani pia atakutana na wahanga wa vita vya Maji Maji ambapo zaidi ya watu laki 3 waliuwawa katika mojawapo ya vita vibaya zaidi vya ukoloni.

Itakuwa mara ya kwanza kabisa kwa rais wa Ujerumani kuitembelea Zambia ambayo itakuwa kituo chake cha pili katika ziara hiyo.